Utangulizi

Haya ni maelezo kwa ufupi jinsi ya kutumia application inayoitwa Stock manager & sales register.

Maelezo haya ni kwa ajili ya vitu muhimu kwenye application, application ina vitu vingi zaidi. Kama ukiona kitu hakijatolewa maelezo hapa, usisite kuwasiliana nasi, tutakusaidia kwa iwezekanavyo.

 

Mawasiliano

 

Application hii ni ya bure, inatunza kumbukumbu zako mtandaoni, hivyo inahitaji internet. Lakini usijari kama ukiwa hauko hewani, application itaendelea kufanya kazi bila mtandao, na taarifa zako zitakuwa salama bila shida yoyote. Ukirudi hewani, taarifa zitatunzwa hewani.

Taarifa zako zote zitahusishwa na akaunti yako uliyotumia, hivyo hata ukibadili simu na kuiweka application upya, taarifa zako zote utazikuta zikiwa salama.

 

Kama una ushauri wowote, au kama unataka kitu kiongezwe/kibadilishwe kwenye application, au kama unataka kuchangia mchango wako kwetu, usisite kuwasiliana nasi. Asante sana.